April 6, 2025 10:35:34 AM Menu




KIKOSI cha Yanga kikicheza mchezo wake wa kwanza kwenye ligi kuu, kilifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya African Lyon lakini pia kikapiga pasi nyingi zaidi kuliko wapinzani wake Simba.
Mabao ya Yanga katika mchezo huo yalifungwa na Deus Kaseke, Simon Msuva na Juma Mahadhi aliyesajiliwa msimu huu kutoka Coastal Union ya Tanga ambayo pia imeshuka daraja.
Katika mchezo wa juzi  Yanga inayonolewa na kocha mholanzi Han van Der Pluijm, ilifanikiwa kupiga jumla ya pasi 366 huku Lyon wao wakipiga 150.
Lakini pia Simba ambayo pia ilicheza wikiendi iliyopita dhidi ya JKT Ruvu na kutoka nayo suluhu  ilipiga jumla ya pasi 274 dhidi ya 244 za maafande hao.

29 Aug 2016

Post a Comment

Emoticon
:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

 
Top