WAKATI sakata la baadhi ya mashabiki wa Arsenal kumpinga kocha Arsene Wenger, kutokana na kutoipa mataji timu hiyo likiendelea, kocha huyo ameomba radhi kwa kutotimiza mahitaji hayo ya mashabiki.
Wenger amenukuliwa akisema: “Najua natakiwa kuwafanya mashabiki wawe na furaha. Naomba radhi kwa kutowatimizia hilo. Hata mimi nasikitishwa sana na kutowafanya wao wafurahi.”
                                                      WENGER



Kauli hiyo imekuja mara baada ya mashabiki kadhaa kubeba mabango yaliyokuwa yameandikwa ‘muda wa mabadiliko’ katika mechi ya juzi dhidi ya Norwich ambapo Arsenal ilishinda bao 1-0.
Wenger ambaye timu yake haijashinda ubingwa wa Premier League kwa miaka 12 sasa aliongeza: “Msimu huu tulitegemea kuwa tutakuwa mabingwa wa ligi kuu, haijatokea ndiyo maana wamekuwa na hasira, mimi pia nina maumivu kama wao.
“Kinachotakiwa ni kujipanga na kurejea kwa nguvu msimu ujao. Ndani ya miaka mitatu iliyopita klabu imepiga hatua.”


Post a Comment

 
Top