April 7, 2025 10:04:34 AM Menu




Mwenyekiti wa Yanga, Yusufu Manji leo alikuwa mmoja kati ya mamia waliojitokeza kwenye msiba wa mfanyakazi wake, deogratius Munish ‘Dida’ ambaye amefiwa na baba yake aitwaje Bonveture Munish.
Manji ambaye ni mwenyekiti wa Yanga alihudhuria kwenye uagwaji  wa mwili katika Kanisa Katoliki, Chang’ombe Polisi jijini Dar ambapo baada ya misa hiyo unatarajiwa kusafirishwa kwenda Kilimanjaro kwa maziko.
Aidha baadhi ya wachezaji wa ligi kuu na wale wa madaraja ya chini walijitokeza kwa wingi kanisani hapo kwa ajili ya kumfariji mchezaji mwenzao huyo ambaye pia anaitumikia timu ya taifa.
Baba yake Dida alifariki mchana wa Jumapili iliyopita wakati mwanaye huyo akiwa uwanjani akiiongoza YAnga kupata ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya African Lyon. Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi AMINA.





31 Aug 2016

Post a Comment

Emoticon
:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

 
Top