Anita na mchepuko

SIRI imefichuka kuwa staa wa Liverpool, Dejan Lovren, hakwenda kwenye michuano ya Euro mwaka huu ili kuilinda ndoa yake.

Mchezaji huyo mwenye uraia wa Croatia aliamua kutokwenda kwenye michuano hiyo baada ya kugundua kuwa mke wake anayejulikana kwa jina la Anita, ana uhusiano na rafiki wake wa zamani anayejulikana kwa jina la Dario Torbic, 26.

Mke huyo na mume tayari wana watoto wawili.

Inaelezwa kuwa wawili hao walikuwa wanajiandaa kuachana na beki huyo alikuwa lazima afanya kitu ili hali hiyo isitokee.

Uhusiano wa beki Dario na mke wa beki huyo ulianza mwezi Desemba mwaka jana  wakati wawili hao walipokutana mjini Zagreb.
 
Anita na Levron


Hata hivyo, inaelezwa kuwa Anita alimwambia Dario aende England na wakakutana kwenye hoteli ya Liverpool.

  Hata hivyo, inaelezwa kuwa Lovren alifahamu mchezo huo na wawili hao waliondoka England mwezi Machi kwa ajili ya kwenye Croatia kuonana na mwanasheria ili kufanya utaratibu wa talaka.

Chanzo kilisema: “Ndoa ya Dejan Anita imekuwa kwenye majaribu makubwa sana kwa muda mrefu huko rafiki wa Lovren akihusishwa na taarifa za kutembea na mwanadada huyo.
 “Anita alimwambia mwanaume huyo kuwa wanakwenda Croatia kwa ajili ya talaka na baada ya hapo watakuwa wakiishi pamoja.

“Lakini tukio hilo lilishindikana kutokana na Anita kuwa mjamzito ndipo Dejan akaamua kupambana na ndoa yake, na kupanga kuwa mwezi Juni anatakiwa kupumzika na mke wake ili kupata suluhisho la matatizo yote jambo ambalo mkewe aliliridhia.”

Inaelezwa kuwa alijitoa kwenye timu ya taifa bila kutoa taarifa yoyote na mwisho aliondolewa kwenye timu hiyo na kuweka chuki kwa mashabiki wa Croatia ambao walikuwa wakimtegemea.


Post a Comment

 
Top