KITENDO cha nahodha na kiungo wa Simba SC, Jonas Mkude kupewa kadi nyekundu (Red), katika mechi yao ya mwisho dhidi ya Yanga SC kimeitikisa timu hiyo kuelekea katika michezo yao inayofuata.
Mkude alipewa kadi hiyo akidaiwa kumsukuma mwamuzi mara baada ya Amissi Tambwe wa Yanga kufunga bao la kuongoza.
Benchi la ufundi la Simba chini ya Mcameroon, Joseph Omog limekiri kuwa na kazi ngumu ya kuziba nafasi ya kiungo mkabaji katika kikosi hicho kwa kumkosa Mkude hasa ukizingatia wana mechi ngumu mbele yao dhidi ya Prisons na Mbeya City mkoani Mbeya.
Kocha Msaidizi wa Simba, Jackson Mayanja alifafanua kuwa ingawa kikosi chao ni kipana na kina wachezaji wengi lakini bado mchango wa Mkude utaendelea kukosekana kutokana na staili yake ya uchezaji.
 “Ndiyo tuna kikosi kipana na wachezaji wazuri lakini bado tuta-miss mchango wa Mkude akiwa uwanjani, inafahamika umuhimu wake. Katika nafasi yake anaweza kucheza Mzamiru (Yassin), Awadh Juma na wengine lakini bado tutaangalia nani atafiti vizuri katika mazoezi ya maandalizi.
“Sitaki kuizungumzia ile kadi aliyopewa maana mwamuzi ana maamuzi yake lakini kivyovyote katika timu lazima itakuwa imegharimu,” alisema Mayanja, raia wa Uganda.

Post a Comment

 
Top