VIDEO Queen na mtangazaji wa kituo cha redio Choice FM, Gift Stanford, maarufu ‘Gigy Money’, amekiri kuwahi kuvuta bangi kama sehemu ya baadhi ya vilevi alivyowahi kutumia.
Gigy Money ameliambia DIMBA Jumatano kwamba, hana sababu ya kuficha kama aliwahi kuwa mtumiaji mzuri wa kilevi hicho kwasababu ni maisha ya ujana ya matukio mengi.
“Niliacha tabia ya kuvuta bangi baada ya kuona nikitumia akili yangu inakuwa kama inavurugika na kuwa sina uwezo wa kusema lolote mpaka pale hali hiyo itakaponitoka kichwani,”alisema msanii huyo mwenye makeke.

“Kila siku mimi nasimamia ukweli, na hilo sina shaka nalo na mara kwa mara nimekuwa hivyo, nimesikia minong’ono watu wanasema navuta bangi lakini ukweli ni kwamba niliwahi kulipuliza sana kabla ya kuacha baada ya kuona naweza kujiharibu akili.”
Alisema, anaamini kwa kusema ukweli huo atakuwa amewafunga midomo wale wote waliokuwa wakivumisha kwamba bado anavuta wakati alishaacha.

Post a Comment

 
Top