KIKOSI cha Simba chini ya Mcameroon, Joseph Omog, kesho Alhamisi kinatarajiwa kusafiri kutoka jijini Dar kwenda Dodoma kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Polisi Dodoma ya mkoani humo.
Mchezo huo wa kirafiki unatarajiwa kupigwa Jumamosi hii kwenye Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.
Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara, alisema wameupokea mwaliko huo kwa mikono miwili kwani kutokana na ligi kusimama, watautumia mchezo huo kwa kukipima kikosi chao.
 “Alhamisi (kesho) timu itaelekea Dodoma kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Polisi Dodoma, tumepata mwaliko huu kutoka katika Chama cha Soka Mkoa Dodoma (Dorefa) chini ya mwenyekiti wake, Mulamu Ng’ambi.
“Tunaunga mkono mpango wa Rais Magufuli wa kuhamia Dodoma na katika mchezo wetu huo, mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na tutabeba bango kubwa kuonyesha kumuunga Magufuli katika mpango wake huo,” alisema Manara.

Post a Comment

 
Top