BOKUNGU KUSHOTO

BEKI wa timu Simba, Janavier Bokungu na kiungo, Mussa Ndusha, bado wataendelea kutoitumikia timu hiyo kutokana na uhamisho wao kimataifa (ITC) kuchelewa.

Katibu wa Simba, Patrick Kahemela, alisema wanaendelea kushughulikia uhamisho wao ili waweze kuitumikia timu hiyo.
“Tuliomba ITC kutoka Darling Club (DC Motema Pembe), lakini hazijafika, tunaendelea kufuatilia na mchezo ujao wanaweza kucheza,” alisema.

Post a Comment

 
Top