VIDEO queen anayezipendezesha video za wasanii mbalimbali wa muziki nchini, Gift Stanford ‘Gigy Money’, amesema thamani ya Wema Sepetu ni kubwa, haifanani na shughuli anazozifanya hivi sasa za kuandaa maonyesho ya ngoma za Uswahilini maarufu kama vigoma.

Gigy Money, ameliambia Papaso la Burudani kuwa ukubwa wa jina la Wema Sepetu linashabihiana kabisa na lile la yule nyota wa Marekani, Kim Kardashian, hivyo mambo hayo ya vigoma yanampoteza kwenye ramani.
“Wema Sepetu ni brand, ni jina kubwa ambalo angelitumia vizuri angekuwa milionea, lakini huenda dharau na kujiona staa leo hii ameangukia kwenye vigoma ambavyo si levo zake,” alisema Gigy Money.

Post a Comment

 
Top