Kocha mkuu wa timu ya Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa amemuita katika kikosi chake kipa wa maafande wa JKT Ruvu, Said Kipao.

Mkwasa kamjumuisha chipukizi huyo kuchukua nafasi ya Deogratius Munishi aliyefiwa na baba yake jana hivyo kushindwa kujumuika na kikosi cha Taifa Stars kitakachoondoka nchini kuelekea Nigeria siku ya Jumatano.

Kipao alionyesha uwezo mkubwa wa kupangua michomo ya Ajib, Mavugo, Kichuya na wengineo.

Amesajiliwa na JKT Ruvu msimu huu kutoka kituo cha kunoa makipa kinachoendeshwa na kipa wa zamani wa Taifa Stars na Yanga, Peter Manyika.

Post a Comment

 
Top