![]() |
|
Emmanuel Mbaga akijiandaa kusaini mkataba
mbele ya viongozi wa Coastal Union.
|
COASTAL Union ambayo msimu wa 2016/17
itacheza Ligi Daraja la Kwanza baada ya msimu uliopita kushuka, imemsajili
kiungo mshambuliaji, Emmanuel Mbaga ‘Samatta’ lakini kubwa ametamba kuirejesha
timu hiyo ligi kuu.
Mbaga ambaye amekuwa akivutiwa na
nyota wa Tanzania anayechezea Genk ya Ubelgiji, Mbwana Samatta amejiunga na
kikosi hicho kwa mkataba wa mwaka mmoja akitokea Klabu ya Opec ya visiwani Zanzibar
amesema amejiunga na Coastal kwa kuwa anaamini ni sehemu sahihi kwake na kwamba
atapambana na wenzake ili kuhakikisha inarejea ligi kuu msimu unaofuata.
Akizungumza na spotiripotablog, Mbaga
alisema, mashabiki hawatakiwi kuwa na hofu kwani yeye na wenzake wamejipanga
kuhakikisha wanaifanya kazi ambayo imewafikisha sehemu hiyo na wanaamini ligi
itaisha kwa furaha.
“Cha muhimu tuombe uzima kwanza kwani
ndiyo kila kitu. Lakini niwaahidia mashabiki wetu kuwa mimi pamoja na wenzangu
tutapigana kuhakikisha tunairudisha timu ligi kuu, makocha wetu ni wazuri na
wamekuwa wakitupa mazoezi mazuri ambayo ndiyo yanayotufanya tujiamini kuwa
tutarejea ligi kuu msimu ujao,” alisema Mbaga ‘Samatta’.



Post a Comment