KIKOSI
cha Simba, juzi asubuhi na jana jioni kilifanya mazoezi yake kwenye Uwanja wa Boko
Veterani jijini hapa, wachezaji wa timu hiyo walionekana kuwa wapo fiti
kutokana na jinsi walivyokuwa wakipambana uwanjani takriban saa mbili bila ya
kuchoka huku wakionyesha uwezo wa juu wa kukaba na kutengeneza nafasi za
kufunga.
Kutokana na hali hiyo kocha mkuu wa timu hiyo, Mcameroon,
Joseph, Omog amesema, safari hii ubingwa ni mali yao, hivyo wapinzani wao
wataisoma namba na amejipanga kuuchukua bila ya kupoteza mchezo wowote kama
alivyofanya wakati akiifundisha Azam FC.
“Nashukuru Mungu tunaendelea vizuri na mazoezi yetu,
lengo letu kubwa ni kuhakikisha tunaibuka mabingwa. Vijana kama ulivyowaona
wapo fiti na tayari kabisa kwa mapambano hata kama wakisema ligi ianze leo
kwani tulipokuwa Morogoro nilijitahidi sana kuwajengea stamina na uwezo wa
kucheza kitimu ndiyo maana wanaonekana kuwa fiti.
“Kilichobakia sasa ni kuwaongezea vitu vichache tu vya
kiufundi na baadaye ni kutafuta ushindi tu kwa kila mechi. Simba ya safari hii
ni tofauti na ya msimu uliopita,” alisema Omog akiungwa mkono na msaidizi wake,
Mganda, Jackson Mayanja.


Post a Comment