STAA wa Real Madrid, Cristiano
Ronaldo ni kama ameamua kujibu mapingo kwa kocha wake wa zamani, Jose Mourinho
kupitia mtandao wa Instagram.
Mourinho ambaye kwa sasa ni kocha wa
Manchester United alimponda Ronaldo kwa kitendo chake cha kutoa maelekezo
kwenye mchezo wa fainali wa Kombe la Euro katika kipindi cha dakika za nyongoze.
Ronaldo aliumia mapema tu kwenye
mchezo huo wa fainali dhidi ya Ufaransa, lakini wakati wa dakika 30 za nyongeza
alisogea kwenye mstari wa makocha na kuanza kuwapa wachezaji wenzake maelekezo
tukio ambalo Mourinho aliliponda na kusema wala halikuwasaidia Ureno kutwaa
ubingwa huo.
Hata hivyo, wikiendi iliyopita Ronaldo
aliweka picha kwenye mtandao wa Instagram akiwa na Bruno Alves, Pepe, Andre
Gomes wakisherehekea ubingwa huo wa Euro na kuandika 'Nakumbushia Mapema',.
Picha hiyo ilipata komenti nyingi
zilizoonyesha kuwa Ronaldo alikuwa akimjibu Mourinho.
“Cristiano Ronaldo hakuisaidia timu,
kulikuwa na wachezaji 11 uwanjani ambao walikuwa wakifanya kazi yao lakini siyo
Ronaldo.
“Mtu aliyekuwa kwenye benchi
akifundisha timu ni kocha siyo Ronaldo, nilimuona kama mtu aliyeshindwa
kujizuia,” alisema Mourinho siku chache zilizopita.
Post a Comment