BAADA ya kikosi
cha Kagera Sugar kinachoshiriki Ligi Kuu Bara kukubali kichapo cha bao 1-0
kutoka kwa Alliance kwenye mchezo wa kirafiki uliopigwa Uwanja wa Butimba TTC,
kocha mkuu wa hiyo, Mecky Mexime amesema bado kikosi chake kinajiandaa na
kitakuwa fiti kabla ya ligi kuanza.
Kagera Sugar ipo
mkoani hapa kwa ajili ya michezo kadhaa ya kirafiki na timu zinazoshiriki Ligi
Daraja la Kwanza na Ligi Kuu zilizopo ili kuimarisha kikosi cha timu hiyo.
Mexime alisema pamoja
na kupoteza mchezo huo bado anaimani na kikosi chake kuwa kitafanya vyema msimu
ujao kwenye ligi kuu.
"Tumekuja Mwanza
kwa ajili ya kucheza michezo kadhaa ya kirafiki na timu zinazoshiriki daraja la
kwanza na ligi kuu ili kuangalia upungufu mapema kabla ligi haijaanza kupoteza
mchezo wetu dhidi ya Alliance hilo kwetu hatuoni shida bali upungufu uliojitokeza ndiyo tutakaoufanyia kazi
mapema,” alisema Mexime.
Post a Comment