MENEJA wa
Juventus, Massimiliano Allegri amemtaka kiungo wake, Paul Pogba ambaye
anatakiwa na Man United kurejea haraka kikosini kesho Jumatatu tayari kwa
kuanza mazoezi na wenzake.
Mchezaji
huyo raia wa Ufaransa tangu ilipomalizika michuano ya Euro 2016 alikuwa mapumzikoni
akila bata huko Marekani.
Pogba, 23,
amekuwa akihusishwa na kuhamia Old Trafford kwa bei ya kuvunja rekodi ya dunia
ya ununuzi wa wachezaji ya pauni milioni 100.
Meneja wa
United, Jose Mourinho aliwahi kusema klabu yake imekaribia kumsaini kiungo huyo
lakini mpaka sasa zimebaki tetesi tu!
"Kwa
sasa, Pogba ni mchezaji wa Juventus," amesema Allegri.



Post a Comment