Mechi ya
kirafiki kati ya Azam FC dhidi ya URA ya Uganda ambayo inatarajiwa kupigwa
kesho kwenye Uwanja wa Azam Complex utapigwa saa 1:00 Usiku badala ya saa 10:oo
Jioni kama ilivyokuwa awali.
Viingilio
kwenye mchezo huo vitakuwa Sh 1,000 kwa viti vya kawaida na 3,000 kwa viti
maalumu (V.I.P).
Azam FC
inapenda kuwakaribisha mashabiki wote wa soka kuhudhuria mchezo huo unaotarajia
kuwa mkali na wa aina yake utakaopambwa na burudani safi kutokana na ubora wa
vikosi vyote viwili vinavyocheza soka la kitabuni.
Post a Comment