Mchana wa
leo zimeripotiwa Taarifa za Mshambuliaji Mkongwe wa klabu ya Simba, Musa Hassan
Mgosi kustaafu rasmi soka na kupewa nafasi ya Umeneja wa klabu hiyo.
Blog hii imemtafuta
Mgosi na kumuuliza juu ya taarifa hizo na maelezo yake ni haya: “Kwanza napenda
kukanusha suala lililoandikwa kwenye mitandao la Mgosi kustaafu, Mgosi kama
Mgosi, suala la kustaafu mpira bado sana, Pogba (Paul) atakapostaafu ndipo
atafuatia Mgosi kustaafu”. Amesema Mgosi na kuongeza”
Hata hivyo,
Mgosi ameonesha wazi yuko tayari kufanya kazi yoyote ndani ya Simba hata kama
atakuwa nje ya uwanja, kitu kinachoashiria yuko mbioni kutundika daluga.
“Mimi ni mchezaji wa Simba, ni Mfanyakazi wa
Simba, nipo tayari kufanya majukumu yoyote yanayoihusu Simba, aidha katika
uchezaji au sekta nyingine”.
Mgosi
anayeheshimika ndani ya Simba amesema kutekeleza majukumu mengine nje ya
kucheza ndani ya Simba alishaanza msimu uliopita, lakini hakuna aliyehusisha na
kustaafu soka.
“Kuisaidia
Simba nje ya uwanja nimelifanya hilo toka mwaka jana, lakini mbona
halijaandikwa hivyo, mwaka jana nimekuwa msaidizi wa Mayanja (Jackson),
nilimsaidia kila kitu kama kocha msaidizi”. Amesisitiza Mgosi na kufafanua:
“Unapozungumza mtu kistaafu tuwe na subira, lazima niseme mwenyewe, sio
mitandao iandike, wengine wanaandika wapate comments, likes na kushtusha watu
ambao wananihitaji.”
Blog hii
imemuuliza kama anaamini muda wa kustaafu umefika na yuko tayari kuwa Meneja wa
Simba.
“Sio tatizo,
ni jukumu ambalo nitalifanyia kazi kwa vile ninavyofahamu mimi, ukitaka
kuangalia kiongozi anayeweza kuingoza Simba kwa kila kitu, hakuna mtu ambaye
kwa haraka unaweza kumuangalia zaidi ya Mgosi,
kwasababu ni mtu ninayeheshimika na wachezaji, naheshimika na mashabiki,
naheshimika na viongozi wa Simba, naamini katika sekta yoyote nitakayopewa
Simba, hakuna atayepinga, kwahiyo najivunia klabu yangu ya Simba.”. Ameongeza
Mgosi.
Licha ya
kakanusha kustaafu rasmi, taarifa za ndani ambazo MPENJA SPORTS imezipata ni
kuwa kweli Mgosi anaelekea kustaafu na mechi ya Jumapili dhidi ya URA itakuwa
maalum kwake kuagwa, lakini yeye mwenyewe na uongozi hauko tayari kulizungumzia
kwasababu kuna masuala kadhaa wanajadiliana.
Inaelezwa
keshokutwa Jumamosi, Mgosi atakutana na
viongozi wa Simba kujadili suala la nafasi wanayotaka kumpa ikiwemo kuandaa
mkataba .
MPENJA SPORTS
Post a Comment