Ikiwa ni
siku chache baada ya Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji kumtaka beki Hassan Kessy
kuondoa hofu kwa kuwa siku itafika atacheza, Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya
Simba, Zacharia Hans Poppe amesema huenda beki huyo akaendelea kubaki nje ya
uwanja kwa msimu huu na mwingine.
Hans Poppe alisema
hayo juzi huku akisisitiza, Kessy hawezi kutocheza milele.
Lakini Hans
Poppe amesema kinachomponza Kessy ni ujeuri wa viongozi wa Yanga ambao wanajua
wamekosea, lakini wanataka kuonyesha umwamba.
Akifanya
mahojiano na SALEHJEMBE jijini Dar es Salaam, Hans Poppe amesema Yanga wanajua
wamefanya makosa, lakini wanataka kuonyesha umwamba kama walivyozoea.
“Waliwahi
kutufanyia hivi katika suala la Yondani, safari hii wamerudia na kumsainisha
Kessy wakati akiwa bado na mkataba na Simba.
“Kama hiyo
haitoshi, mkataba wameufikisha TFF, wameusajili na wakatuma Caf. Sasa sisi tuna
kila kitu na ushahidi mwingine wao wenyewe wameupeleka TFF na Caf.
“Kilichotakiwa
ni kuandika barua, nilikutana na Chanji (kiongozi Yanga). Nikamweleza andikeni
barua mimi nitalisimamia hilo. Lakini hakufanya hivyo, wanataka kuonyesha
ujeuri.
“Kama
itaendelea hivi, ninaamini Kessy hatacheza. Na hapa wa kulaumiwa ni wao maana
Simba tupo hapa,” alisema Hans Poppe na alipoulizwa kama wakiandika barua basi
mara moja watamruhusu Kessy, akajibu.
“Wakiandika
barua, basi sisi tuna jibu au majibu ya kuwapa. Sasa yatapatikana kutokana na
barua yao.”
Post a Comment