YANGA sikieni salamu zenu kutoka kwa mbaya wa mabeki wa timu pinzani, Laudit Mavugo raia huyo wa Burundi amesema amejipanga ipasavyo katika kuisaidia timu yake hiyo kufanya vizuri msimu ujao.
Mavugo amesajiliwa Simba msimu huu akitokea Vital’O ya Burundi ambapo hadi sasa amefanikiwa kufunga bao moja katika mechi ya Simba Day, hali ambayo imeamsha hamasa kwa mashabiki wa timu hiyo.
Amesema hawezi kuogopa mabeki wa Yanga siku watakayokutana na timu hiyo katika michuano ya Ligi Kuu Bara msimu ujao unaotarajiwa kuanza kutimua vumbi Agosti 20, mwaka huu.

“Naijua vizuri Yanga, nimewahi kukutana na mabeki wao kama Cannavaro (Nadir Haroub), Kelvin Yondani, hawawezi kunipa tabu na katika utaratibu wa maisha yangu huwa siogopi mtu, nitapambana nao tu. Naweza kuwapenya na nikafanya maajabu,” alisema kipenzi huyo cha mashabiki wa Simba.

Post a Comment

 
Top