PAMOJA
na nafasi finyu waliyobakiza Yanga kufuzu hatua ya nusu fainali kwenye Kombe la
Shirikisho Afrika, rekodi za kikosi hicho dhidi ya timu za Kiarabu kwenye
Uwanja wa Taifa, zinaipa nafuu kubwa kuelekea mchezo wa leo Jumamosi dhidi ya
MO Bejaia ya Algeria.
Takwimu
zinaonyesha tangu 2009, hakuna timu kutoka Ukanda wa Afrika Kaskazini, maarufu
kama nchi za Kiarabu, iliyowahi kupata ushindi pale Taifa na ushindi wao mkubwa
huwa ni sare.
Mabingwa
wa kihistoria Afrika, Al Ahly ya Misri, 2009 waliandikisha rekodi ya kuwa timu
ya mwisho ya Kiarabu kuifunga Yanga nje-ndani ambapo waliichapa bao 1-0 pale
Taifa kabla ya kuifunga tena mabao 3-0 mjini Cairo.
Ukiwa
ni mwaka wa saba sasa, Yanga tayari imekutana na timu nne za Kiarabu lakini
zote zimeshindwa kupata pointi tatu pale Taifa.
Mwaka
2012 ilikutana na Zamalek ya Misri ambapo zilitoa sare ya 1-1, kabla ya mwaka
2014 kuvunja rekodi kwa kuifunga timu ya Kiarabu, Al Ahly kwa bao 1-0. 2015
Waarabu wa Etoile du Saleh nao wakaangukia kwenye mkumbo wa kugawana pointi
pale Taifa kwa sare ya 1-1 kabla ya kuwang’ang’ania tena Al Ahly mwaka huu kwa
kufungana bao 1-1.


Post a Comment