MWENYEKITI wa Yanga, Yusuf Manji, ameibuka upya baada ya juzi kutangaza kutaka kuikodi klabu hiyo kwa muda wa miaka kumi ili kuifanya kuja kuwa moja ya klabu kubwa ndani na nje ya nchi.
Juzi Jumamosi Yanga ilifanya Mkutano Mkuu wa Dharura kwa wanachama wa klabu hiyo ambapo Manji alitangaza ombi lake hilo ambalo sasa kazi imebaki kwa Baraza la Wadhamini la Klabu ya Yanga kukubali au la.
“Unajua Yanga ina thamani kubwa kuliko hata fedha nilizokuwa nazo na naamini hakuna tajiri ambaye atakuja kuinunua Yanga kwa sababu ina thamani kubwa na ndiyo maana nimesema siwezi kutaja kiasi cha fedha ambacho nitakitoa kuikodi bali nitakachokifanya ni makubaliano na Baraza la Wadhamini kwa yale ambayo nimeyapanga ikiwemo hizo asilimia 25 za faida kuingia klabuni.”

Post a Comment

 
Top