KOCHA wa Arsenal, ARsene Wenger ameonekana kulichukulia kwa umakini mkubwa suala la usajili wa mlinzi wa kati baada ya kuripotiwa kuwa klabu yake imefikia makubaliano binafsi ya kumsajili beki wa Valencia, Shkodran Mustafi.

Arsenal sasa inahaha kupata mlinzi wa kati atakayeziba nafasi ya Per Mertesacker na Gabriel Paulista ambao wameumia na wanatarajiwa kuwa nje kwa ziadi ya miezi mine kila mmoja.

Baada ya kutumia siku mbili kwaajili ya mazungumzo juu ya dili la mchezaji huyo, hatimaye wakala waa Mustafi amethibitisha kwamba dili sasa lipo mbioni kukamilika, huku Arsenal wakitakiwa kumalizana na klabu ikiwa ndiyo hatua ya mwisho.

"Shkodran na Arsenal wamefikia makubaliano, hatua iliyobaki ni Arsenal kumalizana na klabu yake ," Ali Bulut amesema ambaye ni wakala wa Mustafi.

Post a Comment

 
Top