MWENYEKITI
wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe amesema Vital’O ya Burundi
ni watu waliokosa ustaarabu na ni kama wamevamia jambo kuhusiana na
mshambuliaji Laudit Mavugo.
Vital’O
ilijumuisha jina la Mavugo katika usajili wake mpya msimu ujao na kulipeleka
kwenye Shirikisho la Soka la Burundi (FFB) ikisema bado ina mkataba naye.
Hans
Poppe ameliambia Championi Ijumaa kwamba, Mavugo si mali ya Vital’O kama watu
wanavyoamini, badala yake ni mchezaji anayemilikiwa na Klabu ya Solidarity ya
nchini Burundi.
“Nashangazwa
sana na Vital’O kukosa ustaarabu katika hili, Mavugo si mchezaji wao. Tayari
tumemsainisha lakini tunaendelea na klabu yake ya Solidarity ambayo ndiyo
ilimlea na kwa sheria za Burundi, ndiyo inammiliki.
“Alikwenda
kucheza Vital’O kwa mkataba kama wa miaka miwili hivi. Sasa amemaliza, sisi
tumefika hadi katika shirikisho la Burundi na wametupa maelezo ambayo ni
sahihi.
“Inawezekana
Vital’O walitaka kuongeza naye mkataba na imeshindikana. Sasa itakuwa ni vizuri
sana wakafuata
utaratibu, huyu si mchezaji wao,” alisema Hans Poppe.
Hata
hivyo, Championi Ijumaa lilimtafuta, Rais wa Vital’O, Benjamin Bikolimana
kulizungumzia suala hilo ambapo alisema: “Ni kweli tulikuwa na mpango wa kutuma
jina la Mavugo kwa ajili ya kumtumia katika msimu ujao
lakini leo (jana) asubuhi tumezungumza na Simba kuhusiana na hilo suala.
“Simba
ni ndugu zetu na tumefikia pazuri, hatulitumi tena na sasa tupo kwenye mchakato
wa kukamilisha ITC yake (Mavugo) kwa ajili ya kuichezea Simba msimu ujao na
muda wowote kuanzia sasa tutakamilisha huo mpango.”
CHANZO:
CHAMPIONI



Post a Comment