PAUL POGBA
ambaye ametua Manchester United na kuanza mazoezi hatacheza mchezo wa kwanza
dhidi ya Bournemouth, Chama cha Soka (FA) kimethibitisha.
FA imesema Pogba aliyesajiliwa kwa dau
lililovunja rekodi ya dunia amefungiwa kuitumikia timu yake mchezo wa kwanza wa
msimu wa Ligi Kuu.
Kiungo huyo
mwenye umri wa miaka 23, amerudi Old Trafford akitokea Juventus katika usajili
uliofanyika msimu huu wa majira ya joto kwa Pauni 89.3 milioni, ikiwa ni miaka
minne baada ya Old Trafford na kwenda Turin kwa fidia ya Pauni 800,000.
Hata hivyo,
kiungo huyo anapaswa kusubiri hadi mchezo wa pili wa United kwani hataweza
kuitumikia timu yake katika mchezo dhidi ya Bournemouth utakaopigwa Jumapili.
Mfaransa
huyo amefungiwa baada ya kupata kadi mbili katika mchezo wa Coppa Italia msimu
uliopita, kadi ya pili aliipata katika mchezo wa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya AC
Milan katika fainali.
FA
imethibitisha kupitia akaunti yake ya Twitter kwamba kusimamishwa kwake
kumehamishiwa katika Ligi ya Kuu England na kumfanya kutoshiriki katika mchezo
wake wa kwanza chini ya Kocha Jose
Mourinho.
Habari
kutoka ndani ya United zinasema kulikuwa na uwezekano mdogo kwa Pogba kuanza katika
mchezo huo dhidi ya Bournemouth.
Kocha
Mourinho alipanga kumtompanga, Pogba ambaye alicheza mchezo wake wa mwisho
katika kikosi cha Ufaransa kilichopoteza fainali ya Euro 2016 kwa Ureno Julai
10, akicheza dakika 120 za mchezo huo
jijini Paris na wenyeji kufungwa 1-0.



Post a Comment