Ligi Kuu
England itakuwa na vita kubwa msimu huu kutokana na kuwahusisha makocha
bora duniani kuanzia Jose Mourinho,
Arsene Wenger, Pep Guardiola, Jurgen Klopp, Conte na Claudio Ranieri.
Kocha
Guardiola amewasili kuinoa Manchester City wakati Jose Mourinho ameanza kazi
Manchester United.
Presha ipo
pia kwa Arsene Wenger kufika mwisho wa kileleni kutokana na changamoto iliyopo,
wakati Klopp wa Liverpool na Maurcio Pochettino wa Tottenham wanatarajiwa
kuziimarisha timu zao.
Lakini kocha
wa Chelsea, Conte anafikiriwa kuwa atashindwa kuwa na mafanikio kutokana na
mwajiri wake.
Kocha Conte
ametakiwa na Bilionea anayemiliki klabu hiyo, Roman Abramovich akipewa kibarua
cha kuirudisha timu hiyo kwenye ushindi baada ya kupotea katika ushindani msimu
uliopita.
Mpaka sasa,
Conte amesajili wachezaji wawili lakini kujiamini kwake na mbinu zake
zitasababisha athari Stamford Bridge.
Lakini
inaaminika atakuwa wa kwanza kupoteza kibarua chake kati ya makocha sita
wakubwa waliopo Ligi Kuu msimu huu.
Conte
amepewa wastani wa 7/2 akifuatiwa na, Klopp, Wenger, Mourinho, Guardiola na
Pochettino kuondoka katika klabu zao.
Waliopiga
kura wanahofia Conte atakuwa akilengwa na mikono ya Abramovich labda kama Chelsea itaanza msimu kwa kasi.
Bosi wa
Liverpool Klopp na kocha mpya wa Old Trafford, Mourinho watafuata wakiwa na
wastani 4/1 – na kocha wa Arsenal
Wenger, Pochettino na Guardiola wakiwa
na wastani wa 5/1.


Post a Comment