JOTO la
mechi ya Ngao ya Jamii kati ya Azam na Yanga linazidi kupanda, baada ya kocha
wa Azam, Zeben Hernandez, kusema nguvu zake zote anaelekeza katika pambano hilo
litakalochezwa Agosti 17 mwaka huu, kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es
Salaam.
Mechi hiyo
itakuwa ya kwanza kwa Hernandez kucheza na Yanga aliyeanza kuifundisha Azam
baada ya aliyemtangulia, Stewart Hall kuachia ngazi.
Azam kabla
ya kuvaana na Yanga wanatarajia kujipima
nguvu kwa URA ya Uganda katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa utakaochezwa
kesho kwenye Uwanja wa Azam Complex jijini Dar es Salaam.
Akizungumza
na BINGWA jana, Hernandez alisema mechi hiyo itakuwa ya mwisho ya kirafiki
kabla ya kukutana na Yanga kwenye mechi ya kuashiria ufunguzi wa msimu mpya
Ligi Kuu Bara.
“Mechi yetu
na URA itakuwa ni kipimo tosha kwa ajili ya kupambana na Yanga, kwani mawazo yangu ni kushinda na kutwaa Ngao
ya Jamii,” alisema Hernandez.
URA
ilimaliza katika nafasi ya tano katika Ligi Kuu ya Uganda kutokana na pointi
47, huku Azam ilishika nafasi ya pili Ligi Kuu Bara.
Post a Comment