YANGA kwa
mara ya kwanza ikiwa chini ya Kocha George Lwandamina leo Jumamosi inacheza
mechi ya kirafiki na JKU ya Zanzibar kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mbali ya
Lwandamina aliyechukua nafasi ya Hans van Der Pluijm, Yanga pia itacheza kwa
mara ya kwanza kikosini ikiwa na kiungo Justine Zullu na kocha msaidizi Noel
Rodwell Mwandila.
Meneja wa
Yanga, Hafidh Saleh ameliambia Championi Jumamosi kuwa, wamefanya mazoezi kwa
wiki mbili na sasa ni wakati wa kutazama kile walichofanya.
“Kikosi kipo
vizuri na maandalizi yote ya mechi hii yapo sawa, tunataka kupima kikosi chetu
tunaomba mashabiki wetu waje wengi kutazama kikosi chao kipya,” alisema Saleh.
Yanga
inacheza mechi hii ikiwa imesaliwa na siku tano za kufanya usajili huku
ikielezwa kupanga kutumia mchezo huo kumuaga mchezaji wake kiraka aliyemaliza
mkataba Mbuyu Twite.
Akizungumzia
mchezo huo, Kocha wa JKU, Omar Othman, alisema; “Maandalizi yetu yapo vizuri,
watu wategemee upinzani mkali kutoka kwetu hivyo Yanga wajiandae kwa mchezo wa
mapambano.”
Post a Comment