ARSENAL
imeonekana kuzembea katika mbio zake za kumsajili straika waliyekuwa
wakimfuatilia kwa muda mrefu, Mjerumani Julian Draxler ambaye tayari ameripotiwa
kumalizana na matajiri wa Ufaransa, PSG kwa pauni milioni 38.
Picha
ikimuonyesha straika huyo akiwa anakabidhiwa jezi namba 23 na Meneja wa PSG, Patrick
Kluivert imeonekana kwenye vyombo vya habari vya Ulaya nusu saa iliyopita.
Arsenal walitajwa
mara kwa mara kumtaka kiungo mshambuliaji huyo ambaye amejiunga na PSG
akitokea, Wolfsburg ya Ujerumani.
Kiungo
mshambuliaji huyo alijiunga na Wolfs mwaka 2015 akitokea Schakle 04, ambapo
amefanikiwa kuichezea mechi 34 na kufunga mabao sita.
Post a Comment