SIMBA imefuta ratiba ya kuwa na mchezo wa kirafiki wa kimataifa ambao walipanga kukipiga na Wazambia wa Power Dinamo FC, Jumatatu ijayo kwa kile kilichoelezwa ni bajeti kubwa ya mchezo wenyewe.

Katibu wa Simba, Patrick Kahemele amethibitisha hilo kwa kusema sasa siku hiyo ya Jumatatu wamepanga kukipiga na Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Taifa au Uhuru jijini Dar na kusisitiza kuwa baada ya kufeli kwa dili la Power Dinamo hawatakuwa na mchezo mwingine wa kirafiki wa kimataifa.


Katika bajeti hiyo, Simba ilitakiwa kutenga shilingi milioni 25 kisha Azam TV ilikuwa tayari kutoa shilingi milioni 20 kwa ajili ya mchezo huo.

Post a Comment

 
Top