KIUNGO mshambuliaji wa Simba, Shiza Kichuya,
amemfunika vibaya straika wa timu hiyo, Laudit Mavugo katika suala zima la
manunuzi ya jezi zao.
Hiyo imetokea siku chache kabla ya jana Simba kucheza
na Ndanda kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona mkoani hapa ukiwa ni mchezo wa
kwanza wa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara.
Championi lilizungumza na baadhi ya
wafanyabiashara wa jezi hizo waliofika mkoani hapa kutokea jijini Dar, ambapo
walisema kwa sasa jezi za Kichuya ndiyo zinauzwa sana mikoani humo kuliko za
Mavugo.
“Zamani tulikuwa tunauza sana jezi za Mavugo,
kama unakumbuka kipindi kile ndiyo ametua alikuwa maarufu sana, lakini kadiri
siku zilivyosonga mauzo yake yakaanza kushuka na sasa tunauza zaidi za Kichuya.
“Hii imetokana na kiwango kizuri anachokionyesha
uwanjani, mashabiki wamempokea vizuri na ndiyo maana amekuwa maarufu zaidi ya
Mavugo,” alisema mmoja wa wauzaji hao.
Post a Comment