MRISHO
Ngassa hivi karibuni mara kadhaa amekuwa akiomba kufanya mazoezi na Yanga
lakini anachomolewa, sasa leo amepanga kuchezea JKU ambayo inacheza mechi ya
kirafiki na Yanga kwenye Uwanja wa Taifa, Dar.
Ngassa
aliliambia Championi Jumamosi kuwa, lengo lake kubwa lilikuwa kufanya mazoezi
na Yanga ili Kocha George Lwandamina amuone na kupata nafasi ya kusajiliwa
lakini amekuwa akizuiwa.
“Viongozi
wanajua mashabiki wakijua nafanya mazoezi kwao halafu kocha akinikubali labda
wanahisi watalazimishwa wanisajili, sasa kesho (leo) nitachezea JKU ili
kumuonyesha kocha wao (Lwandamina) uwezo wangu.
“Ninachotaka
hapa ni kuonyesha uwezo wangu kwa kocha na baadhi ya mashabiki wa Yanga ambao
anadhani nimeisha, naamini nitafanya vizuri na watanikubali,” alisema Ngassa.
Post a Comment