WACHEZJI NA MAKOCHA WA SIMBA |
WATAISHIA kunawa! Hayo ni maneno ya Wekundu wa Msimbazi, Simba, baada ya kurejea kileleni mwa Ligi Kuu Tanzania Bara, ikiwa ni baada ya kiti hicho kukaliwa kwa takribani saa 24 na watani wao wa jadi, Yanga.
Simba imefanikiwa kuwaondoa Yanga kileleni baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Ndanda FC, kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona, mkoani Mtwara, juzi Jumapili.
Kabla ya kurejea kwenye usukani huo, Yanga ndio waliokuwa wamekikalia kiti hicho, baada ya kuifunga JKT Ruvu mabao 3-0 na kufikisha pointi 36, kabla ya Wekundu wa Msimbazi kuwashusha na kuendeleza pengo la pointi mbili baina yao.
Kocha Msaidizi wa Simba, Jackson Mayanja, alisema ushindi walioupata ni mwendelezo wa malengo yao waliyoyaweka kabla ya kuanza kwa ligi.
“Tangu mwanzoni mwa ligi tulishaweka msimamo wetu kuwa kila mechi kwetu ni fainali na tunataka ushindi si wa chini ya mabao mawili kwenye kila mechi, jambo mbalo tumeweza kulitimiza kwenye mechi yetu ya kwanza ya ufunguzi wa mzunguko wa pili…Hakuna wa kutuzuia, yeyote atakayetokea na kuongoza ligi, ajue atakuwa kileleni kwa masaa machache, kwani lazima tutamuondoa. Hali hii itaendelea hadi mwisho wa ligi tutakapotangazwa mabingwa,” alisema.
Alisema mara baada ya kurejea Dar es Salaam wataendelea na mazoezi yao Uwanja wa Boko kwaajili ya mechi yao inayofuata dhidi ya JKT Ruvu kwenye Uwanja wa Uhuru.
Post a Comment