BEKI mkongwe wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, amesema suala la klabu hiyo kuachana na beki kiraka Mbuyu Twite limemuumiza.
Yanga imeachana na Mbuyu baada ya mkataba wake kumalizika na nafasi yake kuchukuliwa na Justine Zulu ‘Mkata Umeme’ aliyejiunga na kikosi hicho juzi kati akitokea Zesco ya Zambia.

Cannavaro alisema ameumizwa na kuondoka kwa Twite kwani tayari walikuwa kama ndugu na alikuwa akimpenda na kudai kuwa hata yeye ukifika muda ataondoka na watu watammisi kama ambavyo yeye anammisi Twite.

“Ni mtu freshi, hana tabu, hata mimi utafika muda nitaondoka, ni mtu ambaye tulizoeana naye, kusema kweli inaniuma sana lakini ndiyo soka, unajua mkiwa kwenye timu mnakuwa kama ndugu, ndiyo ishatokea hiyo hamna jinsi,” alisema Cannavaro na kuongeza: “Kuhusu kuacha pengo kwa kweli sijui nafikiri mwalimu anajua kila kitu.”

Post a Comment

 
Top