NYOTA WA SIMBA WAKISHANGILIA KWENYE MOJA YA MABAO YAO WALIYOFUNGA KATIKA MECHI YA LIGI KUU |
KATIKA hali isiyotarajiwa, makomandoo wa Simba
waliofika mkoani hapa kwa ajili ya kushuhudia mchezo wa timu yao dhidi ya
Ndanda, walifanya tukio la kushangaza siku chache kabla ya mchezo huo uliopigwa
jana kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona.
Tukio hilo ni la kukesha uwanjani hapo kwa siku
nne kwa madai kwamba wanalinda uwanja ili wapinzani wao wasipate nafasi ya
kuweka uchawi na kusababisha kupoteza mchezo kirahisi.
Championi ambalo lilipiga kambi kwa siku kadhaa
mkoani hapa, lilifika uwanjani hapo jana asubuhi na kuwakuta makomandoo hao
wakiwa makini huku wakisema wameulinda uwanja kwa siku nne.
Mmoja wa makomandoo hao ambaye hakupenda kutaja
jina lake, aliliambia Championi Jumatatu: “Unajua kwenye soka, hasa la kwetu
hapa linakuwa na mambo mengi ya ajabu ikiwemo uchawi, hivyo tumeona ni vema
kuulinda uwanja ili kutotoa nafasi kwa wapinzani wetu kufanya mambo yao ya
ajabu.”
Post a Comment