BONDIA wa ngumi za kulipwa nchini, Francis Cheka 'SMG', amesema kuwa atahakikisha
anapambana mpaka dakika ya mwisho katika
pambano lake dhidi ya Vijenger Singh, raia wa India.
Pambano hilo la ubingwa wa Mabara WBO la raundi
12, linatarajiwa kupigwa kwenye Uwanja wa Thyagajar, New Delhi, India.
Cheka alisema kuwa atahakikisha anamchapa
mpinzani wake katika pambano hilo ili kuipa heshima nchi yake, ikiwezekana afie
ulingoni kabisa.
“Najua Watanzania wapo nyuma yangu wakiniombea leo
niweze kuibuka na ushindi na maandalizi ambayo nimeyafanya imani yangu
nitashinda tu.
“Nipo huku na kocha wangu Saleh Komando amekuwa
akihakikisha nafanya vizuri mbele ya mpinzani wangu ambaye ni mgeni katika
medali ya ngumi za kulipwa, hivyo nitamkaribisha kwa kichapo kikali, afe yeye
au mimi ndani ya ulingo ili bingwa apatikane,” alisema Cheka.
Post a Comment