London,
England
MANCHESTER City
leo itakuwa mwenyeji wa Chelsea kwenye mchezo wa Ligi Kuu England maarufu kama
Premier League.
Mchezo huo
unatarajiwa kupigwa kwenye Dimba la Etihad leo saa 9:30 Alasiri. City wapo
nyuma kwa alama moja dhidi ya vinara Chelsea hivyo akishinda atakwea hadi
kileleni na akifungwa inabidi aombee Arsenal ipoteze mchezo wake wa leo dhidi
ya West Ham, hiyo pia inaigusa na Chelsea.
Kocha wa
Chelsea, Antonie Conte ameonekana kubadili mfumo na sasa wanatumia zaidi 3-4-3
ambao unaonekana kufiti huku wachezaji wake wakionyesha morali kubwa katika
kila mchezo wanaocheza.http://spotiripota.blogspot.com/
Chelsea
imepoteza michezo miwili pekee huku ikitoa sare mara moja na imeshinda mechi
kumi hivyo ina wastani mzuri kisoka kwani hata ukiangalia kwa upande wa
ufungaji wanaonekana kuwa vyema kutokana na straika wake Diego Costa kuonekana
yupo ‘On fire’ na mpaka sasa katupia kambani mabao 10 sawa na Aguero wa City.
City chini
ya Kocha Pep Guardiola, nao siyo wa kubeza kwani licha ya kuonekana kama
wameshindwa kupata matokeo ya ushindi katika mechi kadhaa zilizopita bado huwezi
kusema wanapigwa mchezo wa leo.http://spotiripota.blogspot.com/
Takwimu zao
zinaonyesha katika michezo 13 waliyocheza wameshinda tisa, sare mitatu huku wakifunga
mabao 29 na wao wakiruhusu 12 hivyo siyo wa kubezwa.
Kifuatacho
ni kikosi cha kwanza kinachoundwa na wachezaji wa timu hizi ambazo leo
zitanapambana; http://spotiripota.blogspot.com/
Post a Comment