April 6, 2025 10:17:08 AM Menu



Msanii wa Bongo Fleva Ali Kiba jana Jumamosi alikuwa nchini Uganda kucheza mchezo wa Hisani kwa ajili ya kuchangia mfuko wa kusaidia wa mama wajawazito ambao unajulikana kama Dorah Foundation.

Alikiba akiwa katika mchezo huo wa soka wa hisani uliyowahusisha mastaa mbalimbali, upande wake wa The Celebrity White Team waliibuka na ushindi wa mabao 4-1, huku Ali Kiba akiwa kahusika katika upatikanaji wa bao la pili katika ushindi huo.

Upande wa timu ya Ali Kiba alikuwa na staa wa soka aliyetamba na Simba na Yanga, Emmanuel Okwi, ambapo mchezo ulimalizika na Ali kiba katika mchezo huo wa hisani alipewa Tuzo ya The Best Celebrity Player Award, kama hufahamu ukiachana na muziki Ali Kiba pia ana uwezo wa kucheza mpira.
18 Dec 2016

Post a Comment

Emoticon
:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

 
Top