STARIKA
aliyejiunga na Yanga msimu huu akitokea FC Platinum ya Zimbabwe, Obrey Chirwa
raia wa Zambia, anadaiwa kuendelea kufanyiwa mpango wa kurejeshwa kwa mkopo
katika timu yake hiyo ya zamani ili nafasi yake iweze kuchukuliwa na Mzambia
mwenzake, Winston Kalengo, anayekipiga katika timu ya Leopard ya Congo
Brazaville.
Chanzo chetu
makini kimeeleza kuwa, mabosi wa Yanga wanaendelea kufanya mchakato wa kumtoa
Chirwa kwa mkopo, lengo ni kumpisha Kalengo, ambaye anatarajiwa kudondoka siku
yoyote kuanzia leo ili kuiwezesha klabu hiyo kujiweka sawa zaidi kwenye upande
wa upachikaji wa mabao.
“Kuna jambo kweli
linaendelea ndani ya klabu ambapo viongozi wetu wakuu tangu jana walikuwa
wanaendelea kufanya mipango ya kumuombea Chirwa ili aende kwa mkopo FC Platnaum
na lengo lao kubwa ni kumshusha yule straika anayekipiga Congo.
“Ujue Yanga bado
haijitoshelezi sana kwenye safu ya ushambuliaji na ndiyo maana utaona wanafanya
juu chini ili waweze kuongeza watu wa nguvu kwenye nafasi hiyo, kwani uwezo wa
Chirwa bado haujawavutia kiasi hicho, ,” kilisema chanzo hicho.
Chirwa ambaye
alianza vibaya ndani ya Yanga kiasi kuonekana ni mzigo, katika mechi za mwisho
mwisho za kumaliza mzunguko wa kwanza alionyesa kiwango kizuri na kufanikiwa
kufunga mabao manne kwenye ligi mpaka sasa.
Post a Comment