SIMBA
inamtaka beki wa kulia wa Prisons, Salum Kimenya na hii si mara ya kwanza, sasa
wanavutana kwani beki huyo anataka dau la Sh milioni 80 lakini Simba inazo Sh
milioni 30 tu. Wamekwamia hapo.
Mabeki wa
zamani wa Simba na Yanga, Boniface Pawasa na Bakari Malima wameipa Simba
mchongo kuwa, kama wakimpata beki huyo mambo yao yatakuwa mazuri hata kutwaa
ubingwa wa Ligi Kuu Bara.
Ni hivi,
Simba inataka kumaliza tatizo la beki wa kulia kwani ina mpango wa kumtumia
Janivier Bokungu kama beki wa kati kutoka kulia japokuwa taarifa zaidi zinasema
pia inaweza kumtema mkabaji huyo.
Kimenya yeye
anasisitiza kuwa ni mwajiriwa wa Jeshi la Magereza hivyo ili ajiunge na Simba
ni lazima aiteme ajira yake ndiyo maana anataka dau la Sh milioni 80 vinginevyo
hawezi kuchezea ajira yake.
Kimenya
alisema; “Unajua mimi hapa Prisons nipo kwenye ajira, siwezi kuacha kazi yangu
kwa Sh milioni 30 yaani nitakuwa nimefanya kosa kubwa sana.
“Sitaki
yanikute yaliyowakuta baadhi ya wachezaji walioacha kazi hapa na kwenda
kujiunga na hizo timu, naweza kuacha kazi halafu huko nikakaa msimu mmoja,
unaofuata nikafungashiwa virago, sasa nitakuwa nimefanya nini?
“Kama Simba
wananitaka kweli wanipate fedha nzuri nikawafanyie kazi ambayo wataridhika
nayo,” alisema Kimenya.
Pawasa na
Malima walisema kuwa kama kweli Simba wana nia ya kumsajili Kimenya basi
wafanye kweli kwani atawasaidia kwa kiasi kikubwa.
“Binafsi
namjua vizuri sana Kimenya, nimekuwa nikimfuatilia kwa karibu sana, ni mchezaji
mzuri ambaye uchezaji wake ni kama wa Shadrack Nsajigwa, siyo mtu wa kutaka
tamaa pia ni mpambanaji anayetaka ushindi muda wote,” alisema Pawasa ambaye pia
ni mchambuzi wa michezo katika gazeti hili.
Kwa upande
wake Malima ambaye pia ni mchambuzi katika gazeti hili, alisema: “Kimenya ni
beki mzuri pia ana uwezo wa kucheza nafasi nyingi uwanjani, kama Simba wanata
kumsajili, binafsi nawashauri wafanye kweli atawasaidia sana.”
Simba
wamekuwa wakifanya siri kuhusu mipango yao ya kumsajili Kimenya ambaye
anamaliza mkataba mwishoni mwa msimu huu, lakini Championi Jumamosi linafahamu
uwepo wa harakati hizo.
Post a Comment