MWENYEKITI mpya wa Klabu Azam FC, Iddrisa Nassor ‘Father’
amekata mzizi kuhusu ishu zima za usajili klabu kwao kwa kusema baada ya
kukamilisha usajili wa kiungo wa Mbeya City, Joseph Mahundi wamefunga pazia na
kwamba kilichobakia ni kocha kufanya wanachokihitaji wao.
Father ambaye amechukua cheo hicho, akimrithi Said Mohamed
aliyefariki duniani wiki kadhaa zilizopita baada ya kuugua kwa muda mfupi
amesema kila kitu sasa wanamuachia kocha.
Bosi huyo anasema dirisha hili wameongeza wachezaji wanne
tu; Mahundi anayeungana na Waghana watatu, Mohamed Yahya, Samwel Afful, na
Enock Agyei ambao wote tayari wameishatua kikosini katika maandalizi ya raundi
ya pili inayotarajia kuanza Desemba 17, mwaka huu.
Father alisema baada ya kumaliza kazi yao, sasa limebaki
jukumu la kocha kuwapa matokeo.
Azam ilimaliza raundi ya kwanza ikiwa nafasi ya tatu na
pointi 25, ambapo ilikubali kichapo kutoka kwa timu kama Simba, Ndanda Stand na
Mbao
“Hatutarajii kuongeza mchezaji mwingine baada ya hawa
(Mahundi na Waghana) tumemaliza kazi na kilichobakia ni kazi ya kocha,” alisema
Father.
Post a Comment