PAMOJA na
kumalizana na Mbeya City, bado hakijaeleweka kwa kiungo mshambuliaji, Mrisho
Ngassa ambaye juzi Jumamosi alilazimika kukaa jukwaani kushuhudia timu yake
mpya ikigawana pointi na timu yake ya zamani, Kagera Sugar kwenye mchezo wa
Ligi Kuu Bara.
Ngassa
amesaini mwaka mmoja Mbeya City, lakini juzi alishindwa kuitumikia kutokana na
kutokuwa na Kibali cha Uhamisho wa Kimataifa (ITC), ambacho kimechelewa kufika
kutokana na timu alikotoka, Fanja ya Oman kutokitoa kwa wakati.
Kocha wa
timu hiyo, Kinnah Phiri, ameliambia Championi Jumatatu kuwa, mbali na Ngassa
pia alishindwa kumtumia straika Zahoro Pazzi kwa tatizo kama hilo kutoka katika
timu ya FC Lupopo ya DR Congo, lakini kufikia mchezo ujao dhidi ya Toto
Africans, tatizo hilo litakuwa limetatuliwa.
Aidha,
Phiri amelizwa na kitendo hicho kwa kile alichoamini kwa nafasi
walizozitengeneza, kwa vyovyote vile Ngassa asingekosa mabao kuanzia mawili.
“Tuliwachezea
nusu uwanja, tulitengeneza nafasi zaidi ya 10, lakini ajabu mechi ikaisha
bila-bila, inauma na ninaamini kama Ngassa angekuwemo asingekosa mabao mawili,
japo lazima nikubali (Juma) Kaseja alikuwa msaada mkubwa kwa wenzetu.
“Alitoa
hatari nyingi mpaka kuwafanya washambuliaji wetu kukata tamaa lakini tunajipanga
na mechi zinazofuatia,” alisema Mmalawi huyo.
Post a Comment