Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Simba, Hamisi Kilomoni amemuandikia barua Rais wa Tanzania, John Mgufuli, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda inayohusu kuzuia mkutano mkuu wa wanachama wa klabu hiyo uliopangwa kufanyika Desemba 11, mwaka huu.
Mkutano huo ulilenga kubadili mfumo wa uendeshaji wa timu hiyo kutoka kwa wanachama na kuenda kwa mtindo wa hisa.
“Hivyo mkutano huo hauwezi kufanyika hadi pale watakapokutana na sisi ili tuweze kujadiliana na kufikia makubaliano ndipo tuweze kutoa maamuzi ya kuweza kuendelea na mkutano huo kwani wanatakiwa kufuata katiba na sheria kwani hawajatushirikisha kwa jambo lolote hadi sasa kama bodi ya udhamini.



Post a Comment

 
Top