TAARIFA YA AWALI KIFO CHA MCHEZAJI WA ISMAIL HALFAN WA MBAO FC
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha kushtukiza cha Mchezaji Ismail wa timu ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 20 wa Mbao FC ya Mwanza kilichotokea leo Desemba 4, 2016 kwenye Uwanja wa Kaitaba, Bukoba mkoani Kagera.
Timu hiyo ya Vijana wa Mbao, kama vilivyo timu nyingine 7 za Ligi kuu ya Vodacom, ilikuwa Kituo cha Bukoba katika Ligi ya vijana ambayo kwa msimu huu imefanyika kwa mara ya kwanza. Timu nyingine Nane zilikuwa kituo cha Dar es Salaam.
Ismail aliyeanguka uwanjani dakika ya 74, alipata huduma ya kwanza uwanjani hapo kwa madaktari waliokuwa uwanjani, lakini baadaye taarifa za kitabibu zilionyesha amefariki dunia.
Kamati ya Tiba ya TFF, bado inaendelea na uchunguzi wa kifo cha mchezaji huyo kabla ya baadaye kutoa taarifa za kamili ya kitatibu kujua hasa chanzo hasa cha kifo cha mchezaji huyo ambaye mwili wake umehifadhiwa kwenye Hospitali ya Mkoa Kagera.
Inna Lillah wainna ilayhi Rajiuun. Mwenyezi Mungu, Subb Hanna Watallah ampumzishe mahali pema peponi roho ya marehemu huyu.
Post a Comment