El Clasico ndiyo habari ya leo ambapo wababe wa soka nchini Hispania Real Madrid na Barcelona watakuwa pale Camp Nou kupambana.
Dunia kidogo itasimamisha mambo yake na mashabiki wengi wa soka watatazama mechi ya Ligi Kuu Hispania ‘La Liga’ kati ya Barcelona na Real Madrid kwenye Uwanja wa No Camp leo saa 12:30 jioni.
Hii ni moja kati ya mechi kali za watani wa jadi duniani na inaweza kuwa ya kwanza katika miaka ya hivi karibuni, kwani nyingine sasa zinaonekana ni za kawaida na zilizokosa mvuto. http://spotiripota.blogspot.com/

Mechi ya kwanza ya El Clasico ilichezwa mwaka 1902. Huo ulikuwa mchezo michuano ya Kombe la Ligi ambapo Barcelona ilishinda mabao 3-1, hata hivyo mechi ya kwanza ya La Liga kati ya timu hizo ilichezwa Agosti 17, 1929 ambapo Madrid ilishinda mabao 2-1.
Hadi sasa mechi 264 za El Clasico zimechezwa ambapo Barcelona imeshinda 109, Madrid 97 na zilizobaki 58 ni sare. Ila katika La Liga, Madrid ndiyo vinara kwani katika mechi 172, wao wameshinda 72, Barcelona imeshinda 68 na 32 ni sare.
Hii ni zaidi ya mechi katika La Liga pia kati ya mechi zinazofuatiliwa zaidi Ulaya na duniani kote kila zinapochezwa. Chini ni takwimu mbalimbali zilizowekwa na nyota wa timu hizo zote.

11. Beki na nahodha wa Madrid, Sergio Ramos ndiye kinara wa kadi nyekundu mpaka sasa akiwa kapata 11 na nne kati ya hizo kazichukua kwenye El Clasico.
13. Lionel Messi wa Barcelona ndiye mchezaji mwenye asisti nyingi zaidi katika historia  ya El Clásico akiwa kapiga 13 mpaka sasa. Pia anaongoza kwa kuwa na mabao mengi ambayo ni 21 katika michezo 32 aliyocheza.
21. Katika mabao 21 ambayo Messi amefunga kwenye El Clasico, 12 sawa na 57% amefunga akiwa ugenini yaani pale Bernabeu. http://spotiripota.blogspot.com/
10. Katika mabao 16 aliyofunga Ronaldo kwenye El Clasico 10 kati ya hayo amefunga ugenini yaani Nou Camp lakini pia ana asisti moja katika jumla ya michezo 25 aliyocheza.
18. Nyota wa zamani wa Madrid, Alfredo Di Stefano ndiye kinara wa mabao klabuni hapo katika El Clasico, alifunga mabao 18. http://spotiripota.blogspot.com/
0.Clasico haikuwahi kutoa matokeo ya suluhu kuanzia Novemba 2002 mpaka sasa.

4. Kocha Luis Enrique alishinda mabao 4-0 kwenye mchezo wa mwisho kwenye Uwanja wa Bernabeu na kumfanya kuwa meneja pekee kuwahi kushinda kwa idadi kubwa ya mabao akiwa ugenini dhidi ya Madrid katika La Liga. http://spotiripota.blogspot.com/
23. Matokeo ya mabao 2-1 kwenye Clasico yamejitokeza mara nyingi zaidi ambapo ni mara 43 katika michezo 232 na Madrid wameshinda kwa idadi hiyo mara 23 ambayo ni nyingi zaidi.
21. Barcelona wamefunga bao kila mchezo katika mechi 21 zilizopita dhidi ya Real Madrid, na kuweka rekodi ya kufungwa mfululizo katika historia ya El Clasico.

0. Messi hajawahi kufunga bao kwenye Clasico akiwa anacheza pamoja na Luis Suarez na Neymar.
2. Suarez mchezaji pekee ambaye alifunga mara mbili kwenye Clasico akiwa pamoja na 'MSN' huku Madrid nayo ikiongozwa na 'BBC' kwenye ushambuliaji. http://spotiripota.blogspot.com/

Post a Comment

 
Top