Kikosi cha Yanga |
YANGA imepangwa kucheza na Ngaya Club ya Comoro katika mechi ya
awali ya Klabu Bingwa Afrika lakini kocha wa timu hiyo ya Comoro, Lucien Sylla
Mchangama amesema wao siyo wachovu.
Mechi ya kwanza ya Yanga na Ngaya Club itachezwa kati ya Februari
10 na 12, mwakani na kurudiana kati ya Februari 17 na 19 jijini Dar es Salaam.
Kauli hiyo ya Mchangama imekuja baada ya kila mara timu za
Tanzania kufanya vizuri kila zinapokutana na klabu za Comoro kiasi cha kuwa na
uhakika wa kusonga mbele.
Mwandishi wa Gazeti la Serikali la Al Wattan la Comoro, Elie
Djouma, Mchangama ameliambia Championi Jumamosi kuwa, Mchangama amesema hatokubali
kuona timu yake inafanywa ngazi na Yanga kama ilivyo mazoea ya timu za Comoro.
KIKOSI CHA NGAYA |
“Kocha amesema anaijua historia ya mechi za Yanga na timu za Comoro,
hivyo hatoweza kukubali kufungwa kirahisi nyumbani na hata ugenini,” alisema
Djouma.
Katika kikosi chake, Ngaya Club ambayo inapatikana katika mji
mdogo wa Mde-Bambao, Comoro ambao unapatikana pembeni kidogo ya mji mkuu wa
Comoro, Moroni, ina wachezaji kibao wenye uzoefu.
Ina wachezaji walioichezea Comoro mechi za awali za Kombe la
Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (Chan) ambao ni Said Hachim, Chadhouli
Mdradabi, Salim Ali na Mounir Moussa.
Pia imesajili wachezaji wawili mwezi huu ambao ni Fasoiha Goula
Soilihi and Kamal Djabir. Nahodha wake Said Hachim ni beki tegemeo wa timu ya Taifa
ya Comoro.
Hii ni mara ya tatu kwa Yanga kupangiwa timu ya Comoro, kwani
mwaka 2009 ilicheza na Etoile d'or de Mirontsy na kuifunga jumla ya mabao 14-1
(8-1 na 6-0), mwaka 2010 ikaitoa Komorozine kwa mabao 12-2 (7-0 na 5-2).
Visit this website to Watch Online Naagin 6 Desi Hinsi Serial Full Video In High Quality https://naagin.one/
ReplyDelete