SIMBA imekamatika kwani inadaiwa na Mamlaka ya
Mapato Tanzania (TRA) Sh milioni 500 kama malipo ya kodi ya jengo la klabu hiyo
lililopo Mtaa wa Msimbazi, Kariakoo jijini Dar es Salaam.
TRA iliwasiliana na Simba hivi karibuni na kuwataka
kulipa Sh milioni 500 ikiwa ni malipo ya kodi ya jengo lao hilo ambalo lilikuwa
halilipiwi kwa muda mrefu.
Hata hivyo, Simba wametakiwa kulipa kidogo kidogo
kiasi hicho cha fedha hadi watakapomaliza kitakapokamilika.
Katika ulipaji huo wa kidogo kidogo, Simba
wametakiwa kulipa kiasi cha Sh milioni 45 kila mwezi ili kuweza kulinusuru
jengo lao hilo ambalo ni makao makuu ya klabu hiyo.
Mmoja wa viongozi wa Simba alisema, kwa sasa klabu
hiyo ipo katika wakati mgumu kifedha kutokana na kutakiwa kulipa fedha hizo TRA
kila mwezi ili kulinusuru jengo lao.
“Kuna kipindi TRA walikuja kwa ajili ya kudai kodi
ya jengo letu lililopo Msimbazi ambayo haijalipwa kwa miaka mingi na
kusababisha kufikia kiasi cha Sh milioni 500.
“Tumekubaliana kupeleka kiasi cha Sh milioni 45 kila
mwezi tangu kipindi walichotueleza kama miezi mitatu iliyopita hivyo
tunaendelea na malipo hayo kila mwezi,” alisema kiongozi huyo.
Alipotafutwa Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa
Kodi wa TRA, Richard Kayombo alisema yupo likizo na kuelekeza suala kwa ofisa
mwingine ambaye hakuwa tayari kulizungumzia jambo hilo.
Post a Comment