KIUNGO wa Fanja, Mrisho Ngassa ameibuka na kukana kusaini kwenye kikosi cha Mbeya City.
Ngassa
ambaye hivi karibuni alijiunga na Fanja ya Oman, yupo nchini kwa sasa kwa madai
kuwa anauguza goti ambalo aliumia wakati akiitumikia timu yake hiyo.
Juzi picha
ya Ofisa Habari wa Mbeya City, Dismas Ten akiwa na Ngassa katika moja ya hoteli
maarufu zilizua mjadala mkubwa kuwa nyota huyo wa zamani wa Yanga, Azam na
Simba amemwaga wino Mbeya City.
Picha hiyo
iliwekwa kwenye Instagram na kuisindikiza na maneno yaliyosomeka; “Mnapokamilisha
jambo kutakiana heri ndio uungwana. Kila la heri anko @mrisho_ngasa_17.”
Ngasaa
ameiambia spotiripota kuwa hajasaini Mbeya City isipokuwa picha inayoonekana
aliamua kupiga tu kama picha zingine na kwamba yeye anamilikiwa na Fanja.
"Siyo
kweli, mimi sijasaini huko na hata sijazungumza nao kabisa kuhusu usajili,”
alisema Ngassa.
Post a Comment