Tatizo la Okwi kwishnei Simba
BADO mashabiki wa Simba wanaendelea kumkumbuka straika wao Mganda, Emmanuel Okwi, kutokana na kazi kubwa aliyowafanyia wakati akiitumikia timu hiyo lakini sasa huenda mashabiki wakaanza kumsahau baada ya Juma Luizio kusema atawafanyia makubwa.
Simba imemsajili Luizio kwa mkopo akitokea klabu ya Zesco FC ya Zambia ambapo ametamka wazi kuwa hakuja kutalii bali kufanya kazi na mashabiki wa Wekundu hao wa Msimbazi watarajie makubwa kutoka kwake.
“Nadhani viongozi wa Simba wameona kwamba naweza kuendana na kasi yao ndiyo maana wakakubali nije kuichezea timu yao, binafsi naahidi kwamba nitafanya kila linalowezekana kuonyesha uwezo wangu wote,” alisema.
Alisema anajua kwamba mashabiki wanatamani kikosi chao kitwae ubingwa msimu huu ambapo ametamka wazi kuwa yeye kwa kushirikiana na wenzake watapambana mpaka kieleweke.
Akizungumzia maisha yake ya baadaye alisema wanaodhani kuwa kurudi kwake Tanzania ni kwamba amemaliza maisha nje ya nchi wanajidanganya kwani malengo yake ni kucheza soka barani Ulaya na hilo litatimia.
“Bado malengo yangu ni kufika mbali zaidi, natarajia siku moja nitacheza soka la kulipwa barani Ulaya kwani uwezo huo ninao na pia nina nia hivyo sioni sababu ya kusema nitabakia hapa hapa nchini,” alisema.
Post a Comment