BAADA ya
kupitia mawasilisho ya pande zote kwa njia ya mahojiano, na vielelezo Kamati ya
Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji imebaini mambo yafuatayo ambayo yanapaswa
kuchukuliwa hatua za haraka:
1. Mchezaji
Hassan Hamis Ramadhan au Hassan Kessy alikuwa na Mkataba na Klabu ya Simba
uliokuwa unaishia tarehe 15/06/2016.
2. Young
Africans SC walikiri mbele ya Kamati kupeleka jina la Mchezaji Hassan Ramadhani
Kessy huko Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) tarehe 10/06/2016 huku
mchezaji huyo akiwa ndani ya mkataba na klabu ya Simba.
3. TFF
kupitia Sekretarieti yake ilikuwa na nafasi ya kuweza kuielekeza Young Africans
SC hatua stahiki za kuchukua ikiwa ni pamoja na kuwasiliana na Klabu ya Simba
kama taratibu zinavyoelekeza. Kama hatua hii ingechukuliwa kwa wakati mwafaka
mgogoro huu usingekuwa na sura ya sasa na pengine usingekuwepo.
4. Simba
SC walileta machapisho yanayotokana na Mtandao/blog wa mtu waliomtaja kuwa ni
Bin Zubeiry ukimwonyesha Mchezaji yuko na viongozi wa Young Africans.
5. Young
Africans SC ilionesha Mkataba iliosainiwa na Hassan Hamis Kessy tarehe
20/6/2016 na hivyo hakukuwa na sababu ya msingi ya kufanya mambo yaliyoainishwa
kwenye kipengele cha 2 and cha 4 kabla ya kumalizika kwa mkataba kati mchezaji
Haasan Kessy na Klabu ya Simba.
6. Bila
kuathiri hadhi ya Uanachama wengine wa TFF, Klabu ya Simba ni brand kubwa kama
ilivyo Klabu ya Young Africans, umakini mkubwa upaswa kutumika katika
kushughulikia brand hizi ili kuepuka madhara yasiyokuwa ya lazima.
HATUA:
Kitendo cha
Klabu ya Young Africans kupeleka jina la mchezaji wa klabu nyingine CAF huku
mchezaji huyo akiwa ndani ya mkataba na mwanachama mwingine wa TFF ni kosa
kubwa kwa mujibu wa kanuni za ligi kifungu 69[5] ambalo linapaswa kupewa adhabu
itakayopelekea wanachama wote kuheshimu nafasi ya TFF kwenye suala la usajili
na sio kuanza kwenda CAF au kwingineko ili kulinda integrity ya soka la
Tanzania.
Klabu ya
Young Africans inatozwa faini ya Sh 3,000,000 (Sh milioni tatu) kwa mujibu wa
kanuni na fidia kwa klabu ya Simba ya Sh 50,000,000 (Shilingi milioni hamsini).
Ofisa wa TTF
aliyehusika ama kwa kushirikiana na Uongozi wa Klabu ya Young Africans au kwa
kutochukua hatua stahiki kwa wakati apelekwe kwenye mamlaka yake ya nidhamu,
yaani, Katibu Mkuu wa TFF ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa dhidi yake.
Post a Comment