Luizio kulia

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Juma Luizio, aliyekuwa akikipiga katika klabu ya ZESCO United ya Zambia, aliyetua Simba kwa mkopo, amemchambua kiungo wa Yanga, Jastine Zulu, kwamba ni mchezaji mzuri, lakini anayetakiwa kupewa muda ili kujenga uhusiano na wenzake.
Yanga imemsajili Zulu, ambaye amechukua nafasi ya Meshack Chaila, ambaye ilikuwa chaguo la kwanza la kocha George Lwandamina, lakini ilishindikana kwa kuwa mchezaji huyo amepata ofa Afrika Kusini.

Luizio alisema anamfahamu vizuri Zulu, kwamba ni mchezaji mzuri, kwani ni chaguo la pili kwa aliyekuwa kocha wao, Lwandamina, anapokosekana Zulu.
Alisema Zulu atafanya vizuri sana katika kikosi cha timu hiyo baada ya kuzoea mazingira ya Tanzania pamoja na kuzoeana na wachezaji wenzake.
“Unajua kwa ushindani wa namba uliokuwepo katika kikosi cha Zesco kimesababisha asipate nafasi ya kucheza na kukaa nje kwa muda mrefu, naamini akipata mazoezi hapo atakuwa vizuri,” alisema.

Post a Comment

 
Top